Rais wa mpito wa Burkina Faso
Michel Kafando aliyeondolewa mamlakani na kikosi cha walinzi wa rais
ameachiliwa huru na yuko buheri wa afya, viongozi wa mapinduzi wamesema.
| Kafando alizuiliwa wanajeshi walinzi wa rais walipovamia mkutano wa baraza la mawaziri |
Viongozi hao wa mapinduzi wamekubaliana kuhusu mambo muhimu ya kujadiliwa, huku marais wawili wa mataifa ya Afrika Kusini wakiwasili nchini humo kuongoza mashauriano.
| Sall alipakia mtandaoni picha iliyomuonyesha akiwa kwenye ndege safarini kuelekea Burkina Faso |
Viongozi wa Amerika, Ufaransa na Muungano wa Afrika (AU) wameshutumu mapinduzi hayo.
Watu watatu wanadaiwa kuuawa baada ya wanajeshi wa kikosi hicho cha walinzi maalum wa rais (RSP) kuwakabili waandamanaji katika jiji kuu la Ouagadougou.
Shirika la kijamii lenye ushawishi mkubwa la Balai Citoyen limesema waliouawa ni 10.
Idadi isiyojulikana ya waandamanaji wanaopinga mapinduzi hayo pia wamekamatwa na kuzuiliwa.
Viongozi hao wa mapinduzi wametangaza amri ya kutotoka nje usiku nchini humo na kufunga mipaka yote ya taifa hilo.
No comments:
Post a Comment