Rais wa Marekani Barack Obama
amezungumza na mwenzake wa Cuba Raul Castro kwa njia ya simu, muda mfupi
baada ya marekani kutangaza kuwa imelegeza vikwazo vya kiuchumi dhidi
ya kisiwa hicho.
Vikwazo vya usafiri pia navyo vimelegezwa kwa raia wa marekani.
Rais Castro amezungumzia haja ya kuondolewa kwa vikwazo vyote, lakini bado hajasema ikiwa ataruhusu makampuni ya Marekani kama Mcdonalds na Starbucks kufungua biashara nchini Cuba.
No comments:
Post a Comment