| Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga akisoma hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye maadhimsho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza. |
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akitoa ujumbe maalum kutoka kwa Mkurugenzi
Mkuu wa Unesco, Irina Bokova kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya
Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza.
|
| Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Mwanza. |
| Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi akitoa nasaha zake kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Amani Duniani ambapo kitaifa yamefanyika jijini Mwanza. |
| Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Amani ambapo kitaifa imefanyika jijini Mwanza. |
| Kikundi cha kwaya ya Patimo-Mabatini jijini Mwanza kikitoa burudani kwenye maadhimisho hayo. |
| Burudani ya Qaswida maalum iliyobeba ujumbe wa kutunza 'Amani' ikitolewa. |
| Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Baraka Konisaga akiweka saini kwenye Azimio maalum la kuenzi Amani lililoandaliwa kwenye maadhimisho hayo huku Mgeni rasmi Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Dini mbalimbali la Amani Tanzania (IRCPT), Rev. Canon Godda (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo. |
| Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Charles Mkumbo (kushoto) na viongozi mbalimbali wa dini wakiendelea kusaini Azimio hilo. |
No comments:
Post a Comment