| Abbott alikuwa amekabiliwa na wakati mgumu uongozini |
Mapema Jumatatu, kwenye kikao na wanahabari Canberra, Bw Turnbull alisema iwapo Bw Abbott angesalia kiongozi wa chama hicho, serikali ya muungano ingeshindwa kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Alisema ilikuwa vigumu kwake kufanya uamuzi huo, lakini kwamba ni “wazi kuwa serikali haijafanikiwa katika kutoa uongozi wa kiuchumi unaohitajika” na kwamba Australia inahitaji mtindo mpya wa uongozi.
Bw Turnbull atakuwa waziri mkuu wa nne wa Australia tangu 2013.
Waziri mkuu wa chama cha Leba Julia Gillard aliondolewa uongozini na Kevin Rudd kwenye kura ya uongozi wa chama Juni 2013, miezi kadha kabla ya uchaguzi mkuu ambao chama cha Liberal, chake Tony Abbott, kilishinda.
Bi Gillard mwenyewe alikuwa amemuondoa Rudd kama waziri mkuu 2010.
No comments:
Post a Comment