Picha za wakimbizi wa Syria
waliokwama katika mipaka na vile vile katika vituo vya treni bila kutaja
picha ya mvulana mdogo wa miaka mitatu Alan Kurdi aliyekuwa amesombwa
na maji katika ufukwe wa bahari wa Uturuki zimezua hisia kwa juhudi
zaidi kuchukuliwa ili kuwasaidia wale wanaotoroka vita.
| Wakimbizi wa Syria |
Kufuatia ukosoaji huo,ni muhimu kukumbuka kwamba mataifa hayo ya Uarabuni hayajataka kuwasaidia wakimbizi wa Syria. Ukarimu wa watu binafsi umewasaidia pakubwa wakimbizi hao.
| viongozi wa Uarabuni |
Mataifa ya Uarabuni yametoa takriban dola milioni 900 kupitia kampuni za wahisani pamoja na michango ya watu binafsi.
| Wakimbizi wa Syria |
Mnamo mwaka 2012,wakati vita vya Bashar Al Asaad vilipoanza na kubainisha ushindani mkubwa kati ya mataifa ya Uarabuni yenye wasunni na washirika wao wa Iran,hofu ilianza kuyatawala mataifa hayo kwamba raia wa Syria wanaomtii rais Assad watalazimika kuingia mataifa hayo ya Uarabuni ili kulipiza kisasi.
Sera hiyo haijabadilishwa nchini Qatar,Saudi Arabia ama hata UAE kwa hofu ya uwezekano wa raia walio watiifu kwa rais Assad kulipiza kisasi.
Uvumi umeendelea kuwepo katika mataifa hayo ya kiarabu kwa kipindi cha miaka mitatu kuhusu seli za magaidi wanaokamatwa na kuzuiliwa ijapokuwa hakuna ushahidi wa moja kwa moja wa mpango wa wafuasi wa Assad ambao umeripotiwa.
Idadi ya maelfu ya raia wa Syria wanaotaka kuingia katika mataifa hayo huenda ikaathiri uchumi unaotegemewa na mataifa hayo ili kuweza kufanya kazi.
Kwa mfano,idadi ya raia wa UAE na Qatar iko chini kwa asilimia 10 ya raia wa mataifa hayo.
Idadi kubwa ya raia ni wafanyikazi wanaofanya kazi katika eneo moja hadi jingine.
Wageni huruhusiwa pekee iwapo wake zao ama waume zao wana kazi kamili,hauwezi kusalia katika mataifa hayo ya Uarabuni bila kazi na wakati kandarasi zao zinapokamilika basi wahamiaji wote hulazimika kurudi makwao.
Hivi ndivyo mataifa hayo ya Urabuni yanavyofanya kazi.Kwa hivyo wazo la maelfu ya wageni wanaoingia bila kazi ama bila siku rasmi ya kurudi makwao huyaweka mataifa hayo kati hali isiyo nzuri.
No comments:
Post a Comment