Utafiti wa kampuni moja ya Sweden
uliofanyiwa watu milioni 5 umeonekana kuthibitisha nadharia kwamba urefu
wa mtu na hatari za ugonjwa wa saratani zina uhusiano.
Matokeo yake yalibaini kwamba kwa kila ziada ya sentimita 10,wakati mtu anapokuwa mtu mzima hatari za kushikwa na saratani huongezeka kwa asilimia 18 miongoni mwa wanawake na asilimia 11 miongoni mwa wanaume.
Lakini wataalam walisema kuwa utafiti huo haukuangazia hatari nyingine ambazo watu warefu hawafai kuwa na wasiwasi nazo.
Ripoti za awali za utafiti huo zilizowasilishwa katika mkutano wa wagonjwa wa watoto,watafiti kutoka taasisi ya Karolinska mjini Stockholm walielezea vile walivyolifuatilia kundi moja la watu wazima kwa zaidi ya miaka 50.
Wanawake warefu wana hatari kubwa ya hadi asilimia 20 ya kupatikana na saratani ya matiti huku wanaume na wanawake warefu wakiwa na hatari ya juu ya kupatikana na saratani ya ngozi kwa asilimia 30.
No comments:
Post a Comment