Wafanyakazi wa MSF wauawa Kunduz
Shirika la madaktari wasio na mipaka
la Medecins Sans Frontieres, linasema watatu kati ya wafanyi kazi wake
wameuawa na wengine 30 hawajulikani waliko baada ya zahanati yao
kushambuliwa katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan.
Kulingana na shirika hilo zahanati hiyo iliharibiwa vibaya na mabomu. Shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO linasema kuwa linachunguza kubaini ikiwa shambulizi la marekani lilihusika.
Kumekuwa na mapigano makali katika mji wa Kunduz tangu wapiganaji wa Taliban kuuvamia siku ya Jumatatu.
No comments:
Post a Comment