''Maduka yetu nchini Tanzania na Uganda yanajumlisha asilimia 4.75 ya oparesheni zetu licha ya kutugharimu asilimia 25 ya oparesheni zetu''.
Maduka ya uchumi katika mataifa hayo mawili hayajazalisha faida yoyote katika kipindi cha miaka 5 swala ambalo linalazimu faida zinazopatikana katika maduka ya Kenya kutumika,alisema Kipng'etich.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa tayari maduka hayo yameandika barua kwa Mamlaka ya masoko nchini Kenya ,soko la hisa pamoja na washikadau muhimu kuhusu uamuzi huo na kuongezea kwamba hivi karibuni uchumi itahitaji kuungwa mkono na wamiliki wa hisa ili kuidhinisha mpango huo.
Maduka yote katika mataifa hayo mawili yamefungwa.
No comments:
Post a Comment