Kundi la wanawake nchini Uganda
wanaopinga kuvuliwa nguo kwa mwenzao wakati alipokuwa akikamatwa na
maafisa wa polisi, limefanya maandamano na kujaribu kuelekea bungeni ili
kuwasilisha hoja yao dhidi ya ukatili wa maafisa wa polisi.
Hatahivyo waandamanaji hao walizuiliwa kuendeleza maandamano hayo na kusukumwa hadi katika afisi zao na maafisa wa polisi.
Kulikuwa na jaribio la kuwakamata baadhi yao lakini walikataa.
No comments:
Post a Comment