Mgonjwa mmoja aliyekuwa amebaki ni mtoto wa siku 19 ambaye mama yake alifariki kutokana na ugonjwa huo.msemaji wa kitengo kinachoratibu mapambano dhidi ya Ebola amesema vipimo vilivyochukuliwa mara mbili vimethibitisha kuwa mtoto huyo amepona.
Mwishoni mwa juma lililopita, kundi la watu takriban 70 waliokuwa wamewekwa karantini waliruhusiwa.
Lakini maendeleo haya chanya hayamaanishi kuwa Guinea imefanikiwa, ili kufikia hatua hiyo inapaswa kusiwe na mgonjwa mpya kwa kipindi cha wiki sita zijazo.
No comments:
Post a Comment