Pages

Tuesday, 17 November 2015

Ufaransa na mikakati dhidi ya Ugaidi

Rais wa Ufaransa Francois Hollande
Ufaransa imesema kuwa imedhamiria kutokomeza kitu kinachoitwa makundi ya wapiganaji wa Kiislam,hiyo ikiwa ni kufuatia shambulio la Kigaidi la mwishoni mwa juma.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa atawasilisha mswaada utakaongeza uwigo wa sharia ya kuongezwa kwa muda wa kuwa na hatua za dharula kwa miezi mitatu baada ya kushambuliwa na atapendekeza mabadiliko kadhaa ya katiba.


 Hata hivyo amesema kuwa kampeni za kijeshi dhidi ya IS nchini Iraq na Syria zitaongezwa na kuimarishwa zaidi. Kundi la kigaidi la IS limejitangazia kuwa ndilo lililohusika na mashambulizi hayo katika maeneo ya Bar,Hotelini na kwenye kumbi za starehe, ambapo jumla ya watu 129 waliuawa.

 Akizungumza katika muungano wa Mabunge Hollande amesisitiza kuwa katiba inapaswa kurekebishwa ili kuwa na namna nzuri wanayoweza kuitumia muda wote kuliko kutegemea hatua za dharula tu. Hatua nyingine za Mapendekezo ya Rais ni ongezeko la Polisi 5000 ndani ya miaka miwili ijayo na kuepuka kupunguza bajeti ya vyombo vya ulinzi.

No comments:

Post a Comment