Viongozi wa mkutano wa G20 nchini
Uturuki wamesema wanamipango ya kuweka nguvu zaidi kupambana na vitendo
vya kigaidi hasa kwa kuvunja mianya ya ufadhili wa kifedha kwa makundi
ya kigaidi, Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema njia hiyo inapewa
kipaumbele.
 |
|
Rais wa Urusi, Vladmir Putin ametaka kuzuiwa kwa mianya ya ufadhili kwa IS
|
''Suala la mapambano dhidi ya ugaidi ni moja kati ya
maswala muhimu,hasa baada ya matukio mabaya kama utekaji nyara na vifo
vilivyotokea nchini Ufaransa, kama tunavyoelewa na imekuwa ikizungumzwa
kabla, kuwa njia za ufadhili wa fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi
vikomeshwe,nimetoa mifano kwa taarifa tulizonazo kuhusu watu kutoka nchi
mbalimbali wanaotoa ufadhili kwa wanamgambo wa IS, tumebaini kuwa
ufadhili huu unatoka nchi 40 zikiwemo baadhi za G20''. Alieleza Putin.
Nae
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema kuwa mashambulizi ya Paris
yalikuwa yakipangwa nchini Syria lakini yaliandaliwa nchini
Ubelgiji.Wapelelezi wanashuku kuwa mtu aliyekuwa anasuka mipango hiyo ni
Abdelhamid Abaaoud, mwenye miaka 27, mbelgiji mwenye asili ya morocco,
anatoka katika wilaya ya Molenbeek.
Polisi nchini Ubelgiji
wamewashutumu watuhumiwa wawili na wanamtafuta Salah Abdeslam, raia wa
ufaransa aishie mjini Brussels ambaye nduguye anaaminika kuwa alijitoa
muhanga mjini Paris.
No comments:
Post a Comment