Pages

Friday, 26 August 2016

KUTOKA VIKINDU: Majambazi zaidi ya 10 wakamatwa, wakiwemo askari na Kanali Mstaafu

Image result for aka 47Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani.  

Mwamndishi wetu kutoka eneo la tukio amesema imeshuhudia magari ya polisi (difenda) zaidi ya 16 yakifika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.

Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru njia zimefungwa kutokana na mapambano hayo.


Inadaiwa wamekamatwa majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu. Kiongozi wa wahalifu wao anadaiwa kuwa Kanali wa Jeshi mstaafu.