Pages

Friday, 26 August 2016

Dar: Kijana apanda juu ya daraja Ubungo na kutaka kuonana na Mkuu wa Mkoa la sivyo atajiua

14067689_1077927052296508_7273464591102074251_n.jpg

Huyu jamaa yupo juu ya daraja la Ubungo Bus Terminal zaidi ya saa 2 akitishia kujiua kwa kujiachia na kuanguka chini. 

14088518_329302140748013_1231767766446198070_n.jpgKatibu wa Chama cha Wafanyabiasha za Mezani katika maeneo ya Stendi ya Mkoa, Ubungo jijini Dar, John Shayo amekusanya umati baada ya kupanda juu kabisa ya daraja jipya lililopo eneo hilo na kutaka kujirusha, akihitaji Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda afike hapo kwani hakutendewa haki.

Tukio hilo lililovuta hisia za wengi lilijiri kwenye Daraja la Ubungo ambapo katibu huyo alitaka afe kwa kuwa anadai hajatendewa haki na alitaka Makonda afike amwelezee shida zake katika suala zima la ufanyaji biashara ndipo aweze kushuka la sivyo angejirusha.

Kundi kubwa la watu lilikusanyika eneo hilo huku polisi na gari lao la zima moto wakitanda wakimshangaa akiwa anazungukazunguka akisema yeye ni Mtanzania anahitaji haki ndipo walimsubiria alipokuwa akimpa mkono ndugu yake kama ishara ya kumuaga wakamvuta na kufanikiwa kumshusha.


Baada ya kushushwa, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kisha akapelekwa katika Kituo cha Polisi cha Ubungo ambapo wafanyabiashara wenzake walidai kwamba alikuwa na mgogoro na mwenzake waliyekuwa wanafanya biashara pamoja.