![]() |
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Doto M.James alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera). Bw. Doto M. James ataapishwa kesho tarehe 01 Septemba, 2016 saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kufuatia uteuzi huo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile atapangiwa kazi nyingine.
