![]() |
VIONGOZI Umoja wa Vyama vya
Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam leo wamewapiga marufuku
wanachama wao kushiriki masuala oyote ya kisiasa hapa nchini ikiwemo
maandamano hususani yaliyopewa jina la Oparesheni ya Umoja wa Kupinga
Udikteta Tanzania (UKUTA) yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) na kupangwa kufanyika kesho Alhamisi, Septemba 1,
2016.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es
Salaam leo Jumatano na Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bodaboda Wilaya
ya Kinondoni, Bw. Leonard Mdede wakati akizungumza na wanahabari na
kusema kuwa, dereva bodaboda yeyote atakayekamatwa akijihusisha na
masuala ya kisiasa au maandamano ya kisiasa atachukuliwa hatua kali za
kisheria na uongozi wa chama hicho.
Aidha Bw. Leonard Mdede amewataka
waendesha bodaboda wote wasibebe abiria yeyote atakakuwa amevalia sare
ya chama chochote cha siasa cha hapa nchini na kusema kwa kufanya hivyo
atakuwa amevunja sheria waliyojiwekea hivyo atawajibishwa ipasavyo kwa
mujibu wa katiba na sheria zao.
