![]() |
Akizungumza mjini Mombasa wakati wa
ufunguzi gati la makontena katika bandari ya Mombasa, Kenyatta alipuuzia
maneno kwamba kuna mvutano wowote na badala yake akasema kuwa nchi hizo
zinasaidiana.
Alisema anaona kwenye vyombo vya
habari kwamba kuna “mgogoro baina yetu, lakini nataka kusema wazi wazi
kwamba Kenya na Tanzania hazina mgogoro wowote baina yao,” alisema.
Kenyatta alisema uchumi wa nchi hizo mbili umefungana kwa miaka mingi na ni kwa ajili ya faida ya watu wa nchi hizo mbili. Alitaja kufunguliwa kwa njia
inayojulikana kama “northern frontier” ambayo itaunganisha bandari ya
Mombasa kupitia mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania, hadi Bujumbura, Burundi njia ambayo itafupisha urefu wa kutoka Bujumbura hadi Mombasa kwa
kilomita 300 nzima.
“Afrika Mashariki haiko katika
mashindano ya wenyewe kwa wenyewe,” alisema Kenyatta. “Afrika Mashariki
inashindana na dunia. Tunataka kujaliana (pale penye mapungufu).
Tunataka tutumie nguvu zetu ili kukua, kuendeleza na kuinua uchumi
wetu,” alisema.
Kutokuwepo kwa Rais John Magufuli wa
Tanzania katika mkutano wa hivi karibuni wa kimataifa na Tokyo mjini
Nairobi kulizusha uvumi kuhusu uhusiano wa nchi za eneo hilo.
Kiongozi huyo wa Tanzania ametembelea
Uganda na Rwanda tu tangu achukue madaraka Oktoba mwaka jana
ukilinganisha na rais aliyemtangulia Jakaya Kikwete ambaye alikuwa
akisafiri sana nchi za nje.
Rais Magufuli pia hakuhudhuria
mikutano karibu mitano ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mkutano wa
shirika la biashara duniani na mikutano mikuu ya AU mjini Addis Ababa na
ule wa Kigali Rwanda hivi karibuni.
