Manchester United imefikia makubaliano kumsajili mshambuliaji Memphis Depay toka PSV Eindhoven ya Uholanzi.
Memphis Depay akiwa amezifumania nyavu
Ada
uhamisho wake inasemekana kuwa kati ya pauni milioni 25 hadi 30 na
atasaini mkataba hadi mwaka 2019 huku kukiwa na nyongeza ya mwaka mmoja
zaidi. Depay anatarajiwa kupimwa afya yake wiki ijayo na atajiunga
rasmi na man united mwezi juni dirisha la uhamisho likifunguliwa rasmi.
msimu huu, depay ameifungia psv bao 21 na kuisaidia kutwaa ubingwa wa holland.
Akithibirisha
kuhama kwa Depay, mkurugenzi wa michezo wa psv Marcel Brands akiongea
kwenye tovuti ya klabu hiyo na kusema wamempa baraka mchezaji huyo
kuhama.
Depay ameichezea Psv jumla ya michezo 104 na kufunga mabao 42.
No comments:
Post a Comment