Mkufunzi wa kilabu ya Napoli Rafael
Benitez ameorodheshwa miongoni mwa makocha wataokumrithi Carlo Ancelotti
katika kilabu ya Real Madrid.
Rafael Benitez
Ancelotti anatarajiwa na wengi kuachana na kilabu hiyo baada ya mechi ya mwisho na Getafe wikiendi hii. Mazungumzo
kati ya Real Madrid na Benitez yanaendelea huku kandarasi ya Benitez
katika kilabu ya Napoli ikitarajiwa kukamilika mwezi ujao,ijapokuwa
hakuna makubaliano yalioafikiwa. Klabu ya West Ham pia iliwasiliana na kocha huyo ambaye aliwahi kuifunza Chelsea na Liverpool.
Carlo Ancelotti
Mkufunzi wa West Ham ambaye anaiandaa West Ham dhidi ya Newcastle
anatarajiwa kuanzisha mazungumzo na klabu hiyo kuhusu hatma yake wiki
ijayo.
Benitez alianza kazi ya ukufunzi katika kilabu ya Real
Madrid B na pia amewahi kuifunza
Valladolid,Osasuna,Etramadura,TenerifeValencia na Inter Milan.
No comments:
Post a Comment