Pages

Saturday, 6 June 2015

FAINALI ULAYA, BARCELONA, JUVENTUS TUMBO JOTO

Straika wa Barcelona, Lionel Messi akionekana mwenye tabasam wakati wa mazoezi na timu yake jana jioni kuelekea fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Barecelona na Juventus.
Neymar Jnr katika mazoezi na timu yake, Neymar atakuwa atacheza mchezo wa kwanza wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Luis Suaez naye akifanya yake wakati wa mazoezi na timu yake.
Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri akizungumza na kikosi chake, ikiwa ni maandalizi ya kuivaa Brcelona kwenye mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakayopigwa katika uwanja wa Olympia leo.
Uwanja wa Olympic mjini Berlin utakaotumika kwenye mchezo huo.


LICHA ya Barcelona kupewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini bado upinzani unaweza kuwa mkubwa kutoka kwa Juventus ambao tayari wana mataji mawili msimu huu.
Timu hizo zinatarajiwa kukutana leo Jumamosi kwenye Uwanja wa Olympia ambapo yoyote itakayoshinda itakuwa imetwaa mataji matatu makubwa msimu huu kwa kuwa kila moja ina mataji mawili mkononi.
Kuelekea mchezo huo, kila upande umeonekana kuwa kwenye maandalizi mazuri. Wakati zinawasili kwenye Jiji la Berlin wachezaji wa pande zote walionekana kuwa kwenye hali nzuri na katika utulivu wa kiwango cha juu.
Kiungo mkongwe wa Barcelona, Andres Iniesta ambaye alikuwa akisumbuliwa na kifundo cha mguu anategemewa kuwa fiti wakati mkongwe mwenzake, Xavi, akitarajiwa kuanzia benchi katika mechi yake ya mwisho kabla ya kuondoka klabuni hapo.
Upande wa Juventus timu ambayo inaundwa na wakongwe wengi, inatarajiwa kumkosa Giorgio Chiellini ambaye ni majeruhi.
Safu ya ushambuliaji ya Barcelona ndiyo gumzo kwa sasa kwa kuwa ushirikiano wa Luis Suarez, Neymar na Lionel Messi unaonekana kuwa fiti na kama Juventus hawatakuwa makini basi umoja huo unaweza kuchangia kuipa Barcelona ubingwa.
Kuonyesha kuwa hawataki kupunguza makali, Barcelona tayari wametangaza kumpa mkataba mpya kiungo mshambuliaji wao, Pedro licha ya kuwa amekuwa hana nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza.

No comments:

Post a Comment