Inadaiwa kipa huyo hataivaa tena jezi ya Man
United na ripoti za England zinadai ameshawaaga wachezaji wenzake,
benchi la ufundi na wafanyakazi wa klabu.
Staa huyo aliyenunuliwa kwa Pauni 18 milioni Juni
2011 na kuwa kipa ghali England, amegoma kusaini mkataba mpya Old
Trafford ambao ungemfanya awe analipwa Pauni 200,000 kwa wiki.
Madrid ilikuwa inasubiri imalize suala lake la kuachana na kocha, Carlo Ancelotti, kabla ya kumgeukia De Gea ambaye atakuwa mbadala wa muda mrefu wa kipa wao, Iker Casillas, ambaye nyakati zinaonekana kumpita.
Kocha wa Man United, Louis van Gaal, ambaye yupo
likizoni Ureno, amekiri hana ubavu wa kumzuia kipa huyo asiondoke kurudi
kwao Hispania.
“Sidhani kama ninaweza kumshawishi abaki kwani
anajua kila kitu ilichonacho Man United. Sihitaji kusema lolote, yeye
mwenyewe anahisi kila kitu. Umewaona mashabiki (wanavyompenda)
inashangaza sana. Atakapoondoka, atapoteza hilo. Ana sifa nyingi.
Inabidi aamue mwenyewe,” alisema Van Gaal.
Licha ya kubembelezwa kiaina na Van Gaal, De Gea
ametoa kauli inayoashiria kwamba ataondoka baada ya kutotaka kuzungumzia
hali yake ya baadaye huku akisisitiza yuko likizo kwa sasa.
No comments:
Post a Comment