Uongozi wa chama hicho umetangaza kuwaita
wachezaji wote nchini katika semina ya siku moja ili kuwapiga msasa
wakati dirisha la usajili likiwa limefunguliwa kwa lengo la kuwazindua
kujua haki zao na kuepuka kuingizwa chaka kama inavyofanywa na baadhi wa
viongozi wa klabu nchini.
Katibu Msaidizi wa Sputanza, Abeid Kasabalala
aliliambia Mwanaspoti, semina hiyo ya siku moja itafanyika jijini Dar es
Salaam ikiwa na lengo la kuwasaidia wachezaji kuzitambua haki zao na
kupewa darasa la kusoma mikataba wanayoingia na klabu zao kabla ya
kuisaini kuepuka kulizwa.
“Kwa sasa tunaendelea na mchakato wa kusaka
wadhamini wa kutusaidia kuendesha semina hiyo ili kuwasaidia vijana
wetu, tumebaini wengi wamekuwa wakiingia mkenge kwa kusaini mikataba kwa
kuonyesha sehemu ya fedha watakazolipwa na eneo la kuweka dole gumba,
lakini hawaisomi na kuielewa mikataba na wamekuwa wakiumizwa sana na
klabu zao,” alisema.
Alisema kwa utafiti wao wa muda mrefu, wamebaini
asilimia zaidi ya 70 ya wachezaji wanasainishwa na kupewa nakala za
mikataba badala ya mikataba halisi kama inavyopaswa, ikiwa na maana
wakati wa usainishwaji zinatakiwa nakala halisi tatu, ya mchezaji, klabu
na ile inayokwenda TFF.
Kiongozi huyo alisema Sputanza imekuwa
ikiwahamasisha wachezaji kujiunga uanachama ili kuwasaidia wanapopatwa
na matatizo kama ilivyomtokea Messi, lakini wamekuwa wakihadaiwa na
ujana, kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza na kulizwa na viongozi wajanja.
Kasabalala alidokeza kuwa, mbali na Messi, chama
chao kina kesi nyingine kadhaa za wachezaji wa Ligi Kuu waliolizwa na
klabu zao na wanazifanyia kazi kuhakikisha wanapata haki zao stahiki,
huku wakiwahimiza wachezaji kutokosa semina hiyo itakapoitishwa wiki
mbili zijazo.
No comments:
Post a Comment