Pages

Thursday, 18 June 2015

Marekani kusajili Wanajeshi zaidi Iraq

Viongozi wawili wa juu katika ulinzi wa Marekani wamesema, hakuna uwezekano kwa Marekani kusajili wanajeshi wapatao 24,000 nchini Iraq mwaka huu.
 
Katibu mkuu wa ulinzi wa Marekani Ash Carter, na Mwenyekiti wa umoja wa wafanyakazi, Jenerali Martin Dempsey, wamesema programu za mafunzo zilizotolewa na Marekani bado hazijaweza kuwavutia wengi kama ilivyotarajiwa.

Hata hivyo wamesisitiza watu zaidi kujiunga kwaajili ya mafunzo ya kijeshi, ili hatimaye waweze kushinda vita dhidi ya Wanamgambo wa Islmamic State.

No comments:

Post a Comment