Kocha wa mwanariadha Mo Farah,
Alberto Salazar amekana shutuma dhidi yake kuhusu matumizi ya dawa
zilizopigwa marufuku michezoni akidai kuwa wanaomshutumu wametoa kauli
za uongo dhidi yake.
| Alberto Salazar |
Uchunguzi wa BBC umedai kuwa Salazar ambaye alikuwa Kocha wa Farah mwaka 2011, alikiuka sheria za kupinga dawa zilizopigwa marufuku michezoni na alimpatia dawa hizo ,bingwa wa mbio za mita 10000 Galen Rupp wa Marekani alipokuwa na umri wa miaka 16 mwaka 2002.
''Nitabainisha na kuwasilisha vielelezo kuhusu jambo hili mapema niwezavyo ili Galen na Mo waweze kuelekeza nguvu zao katika kile wanachokipenda na wamefanya jitihada kubwa kufikia mafanyikio hayo ''Salazar aliiambia Guardian.
No comments:
Post a Comment